Follow by Email

Thursday, August 15, 2013

Kamati ya Bunge yakutana na Uongozi wa Wizara

Mhe. Edward Lowassa (Mb.), Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa pamoja na Wajumbe wa Kamati hiyo wakimsikiliza Mhe. Mahadhi Juma Maalim (Mb.), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa alipokuwa akiwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara kwa kamati hiyo. Kikao hicho kilifanyika katika Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam.

 
Mhe. Lowassa akimsikiliza Mhe. Mahadhi wakati wa kikao hicho. Kulia kwa Mhe. Mahadhi ni Bw. John Haule, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakimsikiliza Mhe. Mahadhi (hayupo pichani)

Baadhi wa Watendaji kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakimsikiliza Mhe. Mahadhi (hayupo pichani) wakati wa kikao kati ya Wizara na Kamati ya Bunge.

Mhe. Mahadhi na Katibu Mkuu wakielezana jambo
No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.