Follow by Email

Sunday, July 21, 2013

Tanzania yadhamiria kushirikiana na New Zealand kukuza sekta ya kilimoWaziri wa Mambo ya Nje wa New Zealand, Mhe. Murray McCully amewasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili kuanzia tarehe 21- 22 Julai, 2013.

 Wakati wa ziara hiyo, Mhe. McCully atafanya mazungumzo na Viongozi wa Kitaifa wa Serikali akiwemo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Peter Pinda (Mb); Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb); Wazri wa Nishati na Madini, Mhe. Prof. Sospeter Muhongo (Mb); na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. William Mgimwa (Mb). 

Mazungumzo yao yanatarajiwa kujikita katika kuimarisha maeneo ya ushirikiano wa kiuchumi kati ya Tanzania na New Zealand. Tanzania ina lenga kujifunza kutoka New Zealand kutokana na nchi hiyo kupata mafanikio makubwa katika sekta ya kilimo hususan ufugaji na viwanda vya kusindika maziwa na mazao mengine.
Eneo lingine ambalo Tanzania inataka kushirikiana na New Zealand ni sekta ya nishati mbadala. Tanzania imedhamiria kukarabisha makampuni ya New Zealand kuwekeza nchini katika uzalishaji wa nishati ya nguvu ya jua na geothermal.

Kukaribishwa kwa makampuni hayo ni moja ya mikakati ya Serikali ya kufikia lengo lake la kuwapatia umeme asilimia 30 ya wananchi wa vijijini ifikapo mwaka 2015.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.