Follow by Email

Monday, July 1, 2013

Rais Barack Obama awasili nchini kwa ziara ya kitaifa

Ndege iliyombeba Rais wa Marekani, Mhe. Barack Obama maarufu kama "AIR FORCE ONE" ikionekana kwa mbali  angani tayari kwa kutua kwenye ardhi ya Tanzania.

Ndege iliyombeba Mhe. Rais Obama ikiwa tayari imewasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam huku Waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari vya nje na ndani ya nchi wakijiandaa kushuhudia tukio hilo la kihistoria.

Mhe. Rais Obama na Mkewe Mama Michelle Obama pamoja na watoto wao wakiteremka kwenye ndege kwa furaha mara baada ya kuwasili nchini kwa ziara ya kitaifa ya siku mbili kuanzia tarehe 1 hadi 2 Julai, 2013.

Mhe. Rais Obama akiwa na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na mkewe Mhe. Mama Salma Kikwete na Mama Michelle mara baada ya kupokelewa.
Mhe. Rais Kikwete na Mhe. Rais Obama wakitembea kwa pamoja.

Mhe. Mama Salma Kikwete na Mhe. Mama Michelle Obama wakitembea kwa pamoja.
Mhe. Rais Obama na Mhe. Rais Kikwete wakisikiliza nyimbo za Mataifa yao zilizopigwa kwa Heshima ya Rais Obama.

Mhe. Ali Mohammed Shein, Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Mizengo Pinda, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Salma Kikwete, Mama Michelle Obama  na Viongozi wengine wa Serikali wakiwa Uwanjani hapo wakati wa mapokezi.

Mhe. Rais Obama akikagua Gwaride la Heshima.

Mhe. Rais Obama akiongozana na Mkuu wa Majeshi wa Tanzania, Jenerali Davis Mwamunyange mara baada ya kukagua gwaride la heshima.

Mhe. Rais Obama akisalimiana na Mhe. Rais Shein.

Mhe. Rais Obama akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.).
Mhe. Membe akiondoka Uwanjani mara baada ya mapokezi.

Mhe. Rais Obama na Mkewe Mama Michelle wakifurahia burudani ya ngoma iliyokuwa ikitolewa uwanjani hapo wakati wa mapokezi yao.


Waandishi wa Habari kazini!

Sehemu ya Wananchi wa Dar es Salaam waliojitokeza kumpokea Mhe. Rais Obama.


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.