Follow by Email

Wednesday, June 26, 2013

Wakuu wa Nchi waanza kuwasili kwa ajili ya kushiriki mkutano wa Smart Partnershipt

Mfalme Mswati III wa Swaziland akiteremka kwenye ndege mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere. Mfalme ni miongoni mwa Wakuu wa Nchi na Serikali watakaohudhuria  Mkutano wa Majadiliano kwa Manufaa ya Wote (Global 2013 Smart Partnership Dialogue) utakaofanyika hapa nchini kuanzia tarehe 28 Juni hadi 1 Julai, 2013.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akiongozana na Mfalme Mswati III wa Swaziland mara baada ya kumpokea alipowasili nchini.

Mfalme Mswati III akisalimiana na Mhe. Shamim Nyanduga, Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji ambaye anawakilisha pia Swaziland mara baaada ya kuwasili.

Mhe. Dkt. Bilal akiongozana na Mfalme Mswati III pamoja na Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa mara baada ya kumpokea Kiongozi huyo.

Mhe. Dkt. Bilal akizungumza na Mfalme Mswati III.

Mhe. Membe akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu ziara ya Mfalme Mswati III.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.