Follow by Email

Wednesday, June 26, 2013

Rais wa Sri Lanka kuwasili nchini kesho


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Sri Lanka, Mhe. Mahinda Rajapaksa anatarajiwa kuwasili nchini tarehe 27 Juni, 2013 kwa ziara ya kitaifa ya siku mbili.

Siku ya kwanza ya ziara yake, Mhe. Rajapaksa atafanya mazungumzo rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete na  kushiriki Dhifa ya Kitaifa.

Tarehe 28 Juni 2013, Mhe. Rajapaksa atatembelea Hekalu la Kibudha lililopo Upanga, Jijini Dar es Salaam lililojengwa na Sri Lanka miaka 93 iliyopita.

Aidha, Mhe. Rajapaksa anatarajiwa kushiriki katika Jukwaa la Ushirikiano kwa Manufaa ya Wote (Global 2013 Smart Partnership Dialogue) utakaofanyika kuanzia tarehe 28 Juni hadi 01 Julai 2013. Ataondoka nchini tarehe 29 Juni 2013 kurejea nchini kwake.


IMETOLEWA NA: WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA, DAR ES SALAAM

26 JUNI, 2013No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.