Follow by Email

Thursday, June 27, 2013

Rais wa Sri Lanka awasili nchini kwa ziara ya kitaifa
Rais wa Sri Lanka, Mhe. Mahinda Rajapaksa akiteremka kwenye ndege mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo tarehe 27 Juni 2013. Mhe. Rajapaksa yupo nchini kwa  ziara ya kitaifa ya siku mbili kuanzia tarehe 27-28 Juni, 2013 pamoja na kushiriki katika Mkutano wa Mahadiliano kwa Manufaa ya Wote (Global 2013 Smart Partnership Dialogue) utakaofanyika hapa nchini kuanzia tarehe 28 Juni hadi 01 Julai, 2013.Mhe. Rais Rajapaksa akiongozana na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete mara baada ya kupokelewa.


Mhe. Rais Rajapaksa  akipokea heshima ya kupigiwa mizinga 21 baada ya kuwasili nchini akiwa na mwenyeji wake Mhe. Rais Kikwete.

Gwaride la Heshima

Mhe. Rais Rajapaksa na mwenyeji wake Mhe. Rais Kikwete wakiangalia vikundi mbalimbali vya burudani (havipo pichani) vilivyokuwepo uwanjani hapo wakati wa mapokezi.

Moja ya vikundi vya burudani vilivyokuwepo uwanjani wakati wa mapokezi ya Mhe. Rais Rajapaksa.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.