Follow by Email

Friday, June 14, 2013

Naibu Waziri amuaga rasmi Balozi wa Ujerumani aliyemaliza muda wake hapa nchini


Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje  Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Dora Msechu akiwakaribisha wageni waalikwa (hawapo pichani) katika hafla fupi ya kumuaga Balozi wa Ujerumani aliyemaliza muda wake wa kazi hapa nchini, Mhe. Klaus-Peter Brandes. Hafla hiyo ilifanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency (Kilimanjaro), Dar es Salaam tarehe 13 Juni, 2013.
Mgeni Rasmi ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Mahadhi Juma Maalim (Mb.) akitoa hotuba wakati wa hafla fupi ya kumuaga Mhe. Balozi Brandes. Pamoja na mambo mengine Mhe. Maalim alimshukuru Balozi Brandes kwa kazi nzuri aliyoifanya hapa nchini ikiwa ni pamoja na kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Ujerumani.
Mhe. Balozi Brandes (katikati) akimsikiliza Mhe. Maalim wakati akitoa hotuba ya kumuaga huku wageni wengine waalikwa wakiwemo Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini wakisikiliza kwa makini


Mhe. Balozi Brandes nae akitoa shukrani zake za dhati kwa Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano iliyoonesha katika kipindi chote alichokuwa hapa nchini.

Mhe. Maalim akimkabidhi Mhe. Brandes zawadi ya picha nzuri ya twiga kama kumbukumbu yake atakapoondoka hapa nchini

Balozi Msechu (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Brandes (kulia kwa Bal. Msechu) pamoja na baadhi ya  Mabalozi na Wakurugenzi  waliokuhudhuria hafla fupi ya kumuaga Balozi huyo.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.