Follow by Email

Thursday, June 27, 2013

Mhe. Membe ampokea Makamu wa Rais wa Botswana


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) (wa kwanza kulia) akiwa na Mwakilishi wa Heshima wa Botswana nchini Tanzania, Bw. Emmanuel Ole-Naiko (wa pili kushoto)  kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere walipokuwa wakimsubiri Makamu wa Rais wa Botswana, Mhe. Ponatshego Kedikilwe kuwasili nchini. Mhe. Kedikilwe ni miongoni mwa viongozi watakaohudhuria Mkutano wa Majadiliano kwa Manufaa ya Wote (Global 2013 Smart Partnership Dialogue) utakaofanyika kuanzia tarehe 28 Juni had 01 Julai, 2013.

Mhe. Kedikilwe akiteremka kwenye ndege mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.

Mhe. Membe akimkaribisha nchini Mhe. Kedikilwe mara baada ya kuwasili.

Mhe. Kedikilwe akikagua Gwaride la Heshima.

Mhe. Kedikilwe na Mhe. Membe wakifurahia burudani iliyokuwepo uwanjani hapo kwa mapokezi.

Mhe. Membe akizungumza na Mhe. Kedikilwe.

Mazungumzo yakiendelea.

Mhe. Membe akimsikiliza kwa makini Mhe. Kedikilwe wakati wa mazungumzo yao.


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.