Follow by Email

Saturday, June 1, 2013

Bunge lapitisha Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) (kushoto) na Naibu wake, Mhe. Mahadhi Juma Maamlim (Mb.) wakijadili jambo kwa pamoja  Bungeni Mjini Dodoma kabla ya kuanza kujibu hoja mbalimbali za Wabunge kuhusu Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa Mwaka 2013/2014 iliyowasilishwa Bungeni hapo tarehe 30 Mei, 2013.

Mhe. Membe akijibu hoja mbalimbali za Wabunge kuhusu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Mhe. Maalim akitoa ufafanuzi kwa baadhi ya hoja zilizotolewa na Wabunge kuhusu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa

Kaimu Mkuu wa Shughuli za Serikali Bungeni na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Samwel Sitta (Mb.) (kulia)  kwa pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Jaji Frederick Werema (katikati), na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Saada Mkuya Salum wakisikiliza kwa makini majibu ya  hoja za Wabunge yaliyokuwa yakitolewa na Mhe. Membe (hayupo pichani)

Waziri Kivuli wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Ezekiel Wenje (Mb.) akiwasilisha Bungeni Hotuba ya Kambi ya Upinzani kuhusu Wizara hiyo.

Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu, Wakuu wa Idara, Vitengo na Taasisi za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakifuatilia majibu ya hoja mbalimbali za Wabunge yaliyokuwa yakitolewa na Mhe. Membe kwa kushirikiana na Mhe. Maalim (hawapo pichani)

Picha zaidi za Wakuu wa Idara kutoka Wizarani na Taasisi za Wizara.

Wakuu wa Idara wakifuatilia kwa makini majibu ya hoja Bungeni

Katibu Mkuu, Bw. John Haule (kulia), Naibu Katibu Mkuu, Balozi Rajabu Gamaha (katikati) na Mkurugenzi wa Idara ya Afrika wakiwa Bungeni

Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jenista Mhagama (Mb.) akiwahoji Wabunge (hawapo pichani) endapo wanaunga mkono Hotuba ya Makadirio ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa mwaka 2013/2014 ambapo asilimia kubwa waliiunga mkono  na kupitisha Bajeti hiyo.

Mhe. Sitta akimpongeza Mhe. Membe mara baada ya Bajeti yake kupitishwa na Bunge.

Baadhi ya Wananchi kutoka Jimbo la Mtama, Mkoani Lindi waliofika Bungeni kumuunga mkono Mbunge wao Mhe. Membe.

Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mhagama akitoka ndani ya Ukumbi wa Bunge mara baada ya kuahirisha kikao.


Waheshimiwa Wabunge wakiwapongeza  Mhe. Membe na Mhe. Maalim mara baada ya Bajeti ya Wizara kupitishwa na Bunge.

Katibu Mkuu, Bw. Haule akimpongeza Mhe. Waziri Membe mara baada ya Bajeti ya Wizara kupitishwa na Bunge.
Wakurugenzi wa Wizara wakimpongeza Mhe. Membe.


Mhe. Membe na Mhe. Maalim wakiwa katika picha ya pamoja na Watendaji wa Wizara na Taasisi mara baada ya Bajeti ya Wizara kupitishwa na Bunge.

Wananchi kutoka Jimbo la Mtama  wakiwa katika picha  ya pamoja na Mhe. Membe.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.