Follow by Email

Friday, May 3, 2013

Rais Rajoelina wa Serikali ya Mpito ya Madagascar awasili nchini kwa ziara ya siku mbili


Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akimkaribisha Mhe. Andry Rajoelina, Rais wa Serikali ya Mpito ya Madagascar mapema jioni ya leo mara baada ya Rais huyo kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.  Rais Rajoelina yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.

Mhe. Rais Kikwete akitembea pamoja na mgeni wake Mhe. Rais Rajoelina wa Serikali ya Mpito ya Madagascar mara baada ya kuwasili nchini jioni hii kwa ajili ya ziara ya siku mbili. Picha na Ikulu (www.issamichuzi.blogspot.com)No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.