Follow by Email

Sunday, May 5, 2013

Rais Kikwete ziarani nchini Kuwait


Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa na mwenyeji wake Mhe. Amiri Sabah Al-Ahmad Al-Jaber Al-Sabah, Mtawala wa Dola ya Kuwait mara baada ya kuwasili nchini humo jana tarehe 5 Mei, 2013 kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku mbili. 

Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Mhe. Amiri Sabah Al-Ahmad Al-Jaber Al-Sabah, Mtawala wa Dola ya Kuwait mara baada ya kuwasili nchini humo jana tarehe 5 Mei, 2013 kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku mbili. 

Katika ziara hiyo, Rais Kikwete ameambatana na Mhe. Bernard K. Membe (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Abdallah Kigoda (Mb), Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Prof. Sospeter Muhongo, Waziriwa Nishati na Madini, Mhe. Nassor Ahmed Mazrui (Mb),Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko wa Serikali ya Mapinduzi – Zanzibar, Mhe. Omar Yussuf Mzee (Mb), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Fedha, Uchumi na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi – Zanzibar.


Picha zote kwa hisani ya www.issamichuzi.blogspot.comNo comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.