Follow by Email

Wednesday, May 29, 2013

Mhe. Membe aongoza kikao cha Menejimenti ya Wizara cha maandalizi ya uwasilishaji wa Bajeti Bungeni

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akiwa na Naibu Waziri, Mhe. Mahadhi Juma Maalim (Mb.) wakipitia Makabrasha kabla ya kuanza kwa kikao na Menejimenti ya Wizara ikiwa ni maandalizi ya mwisho kabla ya uwasilishaji wa Hotuba ya Bajeti ya Wizara kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014 itakayowasilishwa Bungeni tarehe 30 Mei, 2013. Kikao hicho kilifanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara mjini Dodoma tarehe 29 Mei, 2013

Mhe. Membe akiongoza kikao hicho cha maandalizi.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John Haule na Balozi Rajabu Gamaha, Naibu Katibu Mkuu wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani) wakati wa kikao hicho.

Wakuu wa Idara, Vitengo na Taasisi za Wizara wakifuatilia masuala mbalimbali katika makabrasha wakati wa kikao na Mhe. Waziri. Kutoka kulia ni Bw. Dushhood Mndeme, Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Balozi Irene Kasyanju, Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria, Bw. Gabriel Mwero, Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi, Bw. Lucas Suka, Mkuu wa Kitengo cha Ugavi, Bw. Lupakisyo Mwakitalima, Mhasibu Mkuu na Bibi Rehema Twalib, Mkurugenzi wa Taasisi ya Kujitathmini Kiutawala Bora (APRM).

Wakurugenzi wa Idara za Sera na Mipango Bw. James Lugaganya (kushoto), Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (katikati) na Mashariki ya Kati, Balozi Simba Yahya (kulia) wakiendelea na kikao.

Mkurugenzi wa Chuo cha Diplomasia, Balozi Mohammed Maundi (kushoto) na Bw. Andy Mwandembwa, Kaimu Mkuu wa Itifaki wakimsikiliza Mhe. Waziri (hayupo pichani)

Wakurugenzi wakiendelea kupitia makabrasha hatua kwa hatua wakati wa kikao hicho. Kutoka kushoto ni Balozi Bertha Semu-Somi, Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora, Balozi Naimi Aziz, Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda na Balozi Vincent Kibwana, Mkurugenzi wa Idara ya Afrika.

Bw. Omar Mjenga (kushoto), Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Ausralasia na Bw. Khamis Kombo, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Nje Zanzibar wakifuatilia kikao kwa makini

Wajumbe wengine kutoka Wizarani na Taasisi za Wizara wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani) wakati wa kikao hicho. Kushoto ni Bw. Charles Bekoni, kutoka Chuo cha Diplomasia, Bibi Mary Kyando kutoka APRM na Bw. Kombo Hamis

Kikao kikiendelea

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.