Follow by Email

Friday, May 17, 2013

Mhe. Membe amkaribisha nchini Naibu Katibu Mkuu wa Denmark anayeshughulikia masuala ya Maendeleo ya Kimataifa

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), akizungumza na Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia masuala ya Maendeleo ya Kimataifa wa Denmark, Mhe. Charlotte Slente wakati wa hafla fupi ya Chakula cha Usiku kilichoandaliwa na Mhe. Membe kwa heshima ya Mhe. Slente katika Hoteli ya Hyatt Regency (Kilimanjaro) ya Jijini Dar es Salaam. Mhe. Slente alikuwa nchini kwa ziara ya kikazi.

Mhe. Membe akiendelea na mazungumzo na Mhe. Slente huku wajumbe waliofuatana nao kutoka Tanzania na Denmark wakisikiliza.Ujumbe uliofuatana na Mhe. Slente akiwemo Balozi wa Denmark hapa nchini Mhe. Johnny Flento (kulia)

Mhe. Membe akimkabidhi Mhe. Slente zawadi ya picha ya kuchora inayoonesha vivutio vya utalii vya hapa nchini.Mhe. Membe akiagana na mgeni wake Mhe. Slente mara baada ya mazungumzo yao

Mhe. Slente akielezwa jambo na Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Dora Msechu wakati akiagana nae.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.