Follow by Email

Friday, April 26, 2013

Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini washeherekea Miaka 49 ya Muungano


Mhe. Balozi Radhia Msuya akiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Afrika Kusini.

Mhe. Balozi Radhia Msuya (wanne kulia), Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Afrika Kusini akiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Ubalozi (local staff) nchini Afrika Kusini.

Mhe. Balozi Radhia Msuya, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akizungumza katika Sherehe za Muungano nyumbani kwake hivi karibuni, ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Miaka 49 ya Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar. 


Sherehe za Miaka 49 ya Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar zafana mjini Pretoria. Pichani Mhe. Balozi Radhia Msuya akikata keki maalum iliyoandaliwa kusheherekea Sherehe ya Muungano na Wafanyakazi wa Ubalozini na Familia zao hivi karibuni nyumbani kwa Balozi Msuya, nchini Afrika Kusini.


"Kwa raha zetu" ndivyo wakionekana kusema akina Bi. Evaline (kushoto) na Bi. Mary (kulia)wafanyakazi wa Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Afrika Kusini wakisheherekea Miaka 49 ya Muungano.


Mahanjumati ya Muungano.


Mhe. Balozi Radhia Msuya akiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Ubalozi na Familia zao wakati wa wakisheherekea Miaka 49 ya Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika nyumbani kwa Balozi, mjini Pretoria, Afrika Kusini. 

Mhe. Balozi Radhia Msuya akiwa katika picha ya pamoja na local staff wa Ubalozini: Lumbi, Jane, Evaline na Ethel.
Picha zote na Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini 

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.