Follow by Email

Tuesday, April 16, 2013

Katibu Mkuu asaini Mkataba na Mwakilishi wa Heshima wa Tanzania mjini Hamburg


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John Haule kwa pamoja na Bibi Petra Hammelmann, Mwakilishi wa Heshima Mteule wa Tanzania mjini Hamburg nchiniUjerumani wakisaini Mkataba wa kumwezesha Bibi Hammelmann kuwa Mwakilishi wa Heshima rasmi wa Tanzania katika mji huo. Mkataba huo ulisainiwa Wizarani tarehe 16 Aprili, 2013.

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Itifaki katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Andy Mwandembwa (kushoto) pamoja  na Bw. Ali Ubwa, Afisa Mambo ya Nje kutoka Kitengo cha Sheria wakishuhudia uwekaji saini huo.

Bw. Haule na Bibi Hammelmann wakibadilishana mkataba huo mara baada ya kusaini.


Bw. Haule kwa pamoja na Bibi Hammelmann wakionesha mkataba huo.

Bw. Haule akizungumza na Bibi Hammelmann mara baada ya kusaini mkataba utakaomwezesha Bibi Hammelmann kuwa Mwakilishi wa Heshima wa Tanzania mjini Hamburg. Pamoja na mambo mengine Bw. Haule alimhimiza Mwakilishi huyo kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania mjini Hamburg ili kukuza sekta ya utalii hapa nchini.

Bw. Haule akiendelea na mazungumzo na Bibi Hammelmann huku Bw. Mwandembwa na Bw. Ali wakisikiliza.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.