Follow by Email

Tuesday, April 23, 2013

Kaimu Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kikanda azungumza na Mjumbe Maalum kutoka China


Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. David Mwakanjuki (kulia) akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mjumbe Maalum kutoka Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China, Balozi Zhong Jianhua  kuhusu masuala mbalimbali ya  kikanda ikiwemo nafasi ya Tanzania katika utatuzi wa migogoro katika Ukanda wa Maziwa Makuu. Mazungumzo hayo yalifanyika Wizarani tarehe 23 Aprili, 2013.

Balozi Zhong Jianhua naye akimweleza jambo Bw. Mwakanjuki wakati wa mazungumzo yao.

Bw. Mwakanjuki akifafanua jambo kwa Balozi Zhong Jianhua wakati wa mazungumzo yao huku Bw. Charles Faini, Afisa Mambo ya Nje katika Idara ya Asia na Australasia akinukuu mazungumzo hayo.

Wajumbe waliofuatana na Balozi Zhong Jianhua wakimsikiliza Bw. Mwakanjuki.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.