Follow by Email

Sunday, March 24, 2013

Rais Xi Jinping wa China awasili nchini kwa ziara ya siku mbiliRais wa China, Mhe. Xi Jinping na mke wake wakiteremka kwenye ndege mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam kwa Ziara ya Kitaifa ya siku mbili hapa nchini.

Mhe. Rais  Xi Jinping na mwenyeji wake Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiwasalimia baadhi ya kina mama wa Dar es Salaam waliofika Uwanjani hapo kwa ajili ya mapokezi.

Mhe. Rais Xi Jinping na Mhe. Rais Kikwete wakiwa katika Jukwaa Maalum wakati nyimbo za mataifa yao zilipokuwa zikipigwa sambamba na mizinga 21 kwa heshima ya Mhe. Rais Xi Jinping.

Mhe. Rais Xi Jinping akikagua Gwaride Maalum lililoandaliwa kwa heshima yake.

Mhe. Rais Xi Jinping na mwenyeji wake Mhe. Rais Kikwete kwa pamoja na wake zao wakifurahia burudan iliyokuwa ikitolewa  na moja ya viku ndi vya burudani vilivyokuwa uwanjani hapo mara baada ya Rais Xi Jinping kuwasili nchini.

Mhe. Rais Xi Jinping na Mhe. Rais Kikwete wakiondoka uwanjani hapo mara baada ya mapokezi.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.