Follow by Email

Tuesday, March 26, 2013

Rais Xi Jinping wa China akutana kwa mazungumzo na Rais wa Zanzibar na Mhe. MkapaRais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Ali Mohammed Shein akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Xi Jinping walipokutana kwa mazungumzo kuhusu ushirikiano kati ya Tanzania na China katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.

Mhe. Rais Xi Jinping akizungumza na Mhe. Dkt. Shein walipokutana wakati wa ziara ya Mhe. Rais Xi hapa nchini.

Ujumbe uliofuatana na Mhe. Rais Shein wakifuatilia mazungumzo ya Marais hao wawili (hawapo pichani)

Mhe. Dkt. Shein akimweleza jambo Mhe. Rais Xi Jinping wakati wa mazungumzo yao.

Ujumbe uliofuatana na Mhe. Rais Xi Jinping wakati wa mazungumzo na Mhe. Dkt. Shein

Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Benjamin William Mkapa akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Xi Jinping walipokutana kwa mazungumzo maalum katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam wakati wa ziara ya Mhe. Rais Xi hapa nchini.


Mhe. Mkapa akimtambulisha kwa Mhe. Rais Xi Jinping, Mhe. Mahadhi Juma Maalim (Mb), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Mhe. Rais Xi Jinping akisalimiana na Balozi Mbelwa Kairuki, Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa huku Mhe. Mkapa akishuhudia.


Mhe. Xi Jinping akisalimiana na Balozi Celestine Mushy, Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kabla ya kuanza kwa mazungumzo kati ya Mhe. Mkapa na Rais huyo.


Ujumbe uliofuatana na Mhe. Mkapa alipokutana kwa mazungumzo na Mhe. Rais Xi Jinping wa China


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.