Follow by Email

Wednesday, March 20, 2013

Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria akutana kwa mazungumzo na Mkurugenzi wa Idara ya Sheria ya Denmark

Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Irene Kasyanju akizungumza na Mkurugenzi wa Idara ya Sheria katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Denmark, Balozi Thomas Winkler kuhusu ushirikiano kati ya Tanzania na Denmark katika masuala ya  sheria na mikataba mbalimbali  ya kimataifa ikiwemo masuala ya kupambana na Uharamia. Mazungumzo hayo yalifanyika Wizarani tarehe 20 Machi, 2013.

Balozi Winkler akichangia hoja wakati wa mazungumzo hayo huku Balozi Kasyanju akimsikiliza.


Balozi Kasyanju akimsikiliza Balozi Winkler wakati wa mazungumzo yao. Wengine katika picha ni Bw. Elisha Suku (kulia), Afisa Mambo ya Nje katika Kitengo cha Sheria, Wizara ya Mambo ya Nje, Bi. Mille Sofie Brandrup (kushoto), Afisa kutoka Idara ya Sheria za Kimataifa, Wizara ya Mambo ya Nje ya Denmark na Bw. Lars Bo Kirketerp Lund, Afisa kutoka Ubalozi wa Denmark hapa nchini.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.