Follow by Email

Wednesday, March 13, 2013

Mhe. Membe akutana kwa mazungumzo na Waziri wa Biashara wa Ireland


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb), akizungumza na Waziri wa Nchi wa Ireland anayeshughulikia masuala ya Biashara na Maendeleo, Mhe. Joe Costello alipofika Wizarani kwa mazungumzo na Mhe. Waziri Membe kuhusu kukuza  ushirikiano kati ya nchi hizi mbili na pia kuimarisha ushirikiano katika masuala ya biashara na uwekezaji.

Mhe. Membe akiendelea na mazungumzo na Mhe. Costello. Wengine katika picha ni Balozi Dora Msechu (kushoto), Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Balozi Naimi Aziz (kulia), Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda.

Mhe. Membe katika mazungumzo na Mhe. Costello. Wengine katika picha ni ujumbe uliofuatana na Waziri huyo wa Ireland akiwemo Balozi wa Ireland hapa nchini, Mhe. Fionnuala Gilsenan (wa kwanza kulia)

Mhe. Costello akifafanua jambo kwa Mhe. Membe.

Ujumbe wa Ireland wakati wa mazungumzo.

Balozi Msechu (kushoto),  Balozi Naimi (katikati) pamoja na Bi. Zainabu Angovi (kulia) wakisikiliza mazungumzo kati ya Mhe. Membe na Mhe. Costello (hawapo pichani)

Mhe. Membe akijadili jambo na Mhe.  Fionnuala Gilsenan, Balozi wa Ireland hapa nchini huku Mhe. Costello akisikiliza.

Mhe. Membe akiagana na Mhe. Costello mara baada ya mazungumzo yao.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.