Follow by Email

Friday, February 15, 2013

Waziri Membe akutana na Uongozi wa APRM Tanzania

Mhe Waziri leo amekutana na uongozi wa APRM Tanzania. Ujumbe huo chini ya Mwenyekiti Prof. Hassa Mlawa, umetumia fursa hiyo kumshukuru Mhe. Waziri Membe kwa ushirikiano alioutoa yeye kama Focal Point wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wizara kwa ujumla, ikiwemo kulipwa kwa deni la muda mrefu la mchango wa Tanzania katika Sekretariati ya APRM na kuliondolea taifa aibu. Aidha, Ujumbe huo ulitumia fursa hiyo kumueleza Mhe. Waziri juu ya hatua zinazofuata katika utekelezaji wa yatokanayo na Ripoti ya Tathmini ya Tanzania.
Mhe. Membe alipongeza Uongozi wa APRM kwa kazi nzuri waliyoifanya kwa uadilifu mkubwa na kuiletea Tanzania heshima. Ametumia fursa hiyo kuwahakikishia ushirikiano wa Wizara yake katika kuratibu utekelezaji wa yatokanayo na Ripoti hiyo.
Amewataka APRM kusambaza taarifa hiyo kwa wananchi na wadau wote kwa kuwa taarifa hiyo ni ya umma.


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.