Follow by Email

Tuesday, February 19, 2013

UTEUZI WA BODI YA CHUO CHA DIPLOMASIA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Balozi Mwanaidi Sinare Maajar kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Diplomasia (CFR) kilichopo Kurasini Jijini Dar es Salaam.

Aidha, kufuatia uteuzi huo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Kamillius Membe (Mb.) amewateua Wajumbe wa Bodi hiyo kuwa ni:-

1.           Bw. Dushhood M. K. Mndeme
2.           Mhe. Balozi Abdi Mshangama
3.           Mhe. Dkt. Leonidas Mushokolwa
4.           Mhe. Dkt. Harold Utouh
5.           Mhe. Saidi Mtanda (Mb.)
6.           Mhe. Betty Machangu (Mb.)
7.           Bw. Affan Othman Maalim
8.           Bw. Abdurahaman Abdallah

Uteuzi wa Mwenyekiti na Wajumbe hao ni kwa kipindi cha miaka mitatu (3) kuanzia tarehe 22 Januari, 2013 hadi tarehe 21 Januari, 2016.

   
IMETOLEWA NA: WIZARA YA MAMBO YA NJE NA

USHIRIKIANO WA KIMATAIFA, DAR ES SALAAM


15 FEBRUARI, 2013

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.