Follow by Email

Wednesday, February 20, 2013

Rais Mwai Kibaki wa Kenya awasili nchini kwa ziara ya siku mbili


Ndege iliyombeba Rais wa Jamhuri ya Kenya, Mhe. Mwai Kibaki ikiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere huku Viongozi na Wanachi waliofika kumpokea wakishangilia kuwasili kwa Rais huyo nchini. Mhe. Rais Kibaki yupo nchini kwa ziara ya kitaifa ya siku mbili.
Mhe. Rais Kibaki akiteremka kwenye ndege mara baada ya kuwasili ambapo alipokelewa na mwenyeji wake Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Gwaride la Heshima wakati wa mapokezi hayo.

Mhe. Rais Kibaki akielekea kukagua Gwaride la Heshima.


Mhe. Rais Kibaki akikagua Gwaride la Heshima.
 Mhe. Rais Kibaki akiwa na mwenyeji wake Mhe. Rais Kikwete mara baada ya kukagua Gwaride la Heshima.
Mhe. Rais Kibaki pamoja na mwenyeji wake Mhe. Rais Kikwete wakifurahia burudani ya kikundi cha utamaduni kilichokuwepo Uwanjani hapo wakati wa mapokezi
Mhe. Rais Kibaki akiwa na Mhe. Rais Kikwete wakiondoka Uwanjani hapo mara baada ya mapokezi.

Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) (kushoto), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akiwa na Mhe. Sam Ongeri, Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya wakielekea Hotelini kwa mazungumzo mara baada ya mapokezi ya Mhe. Rais Kibaki.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.