Follow by Email

Wednesday, February 27, 2013

Mhe. Membe apokea Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi Mteule wa Uingereza hapa nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akipokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Uingereza hapa nchini, Mhe. Dianna Melrose. Hafla hiyo fupi ilifanyika Ofisini kwa Mhe. Membe, tarehe 27 Februari, 2013.

Mhe. Waziri Membe akionesha Nakala hizo mara baada ya kuzipokea.

Mhe. Membe akizungumza na Mhe. Melrose masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Uingereza mara baada ya kupokea Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi huyo.
Mhe. Balozi Melrose akimsikiliza Mhe. Membe wakati wa mazungumzo yao. Wengine katika picha ni Balozi Dora Msechu (wa pili kutoka kushoto), Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Bi. Zainab Angovi (kushoto), Afisa katika Idara ya Ulaya na Amerika.
Mhe. Membe akimsikiliza Balozi Melrose alipokuwa akifafanua masuala mbalimbal ya ushirikiano.
Mhe. Membe akiagana na Mhe. Balozi Melrose mara baada ya mazungumzo yao.

Picha ya pamoja.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.