Follow by Email

Wednesday, February 13, 2013

Mhe. Membe akutana na Ujumbe wa Wabunge kutoka Ujerumani

Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akiwa na Mhe. Klaus-Peter
Willsch, Kiongozi wa Ujumbe wa Wabunge wa Kamati ya Bajeti ya Bunge la Ujerumani alipokutana nae Wizarani kwa  mazungumzo kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Ujerumani.

Mhe. Membe akimsikiliza Mhe. Willsch wakati wa mazungumzo yao.
Mhe. Willsch (kulia kwa Waziri Membe) akimsikiliza Mhe. Membe wakati wa mazungumzo yao. Wengine katika picha ni baadhi ya Wabunge wa Kamati ya Bajeti ya Bunge la Ujerumani pamoja na Mhe. Klaus-Peter Brandes ( wa sita kutoka kushoto), Balozi wa Ujerumani hapa nchini.

Wajumbe kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakimsilikiza Mhe. Membe (hayupo pichani) wakati wa mazungumzo yake na Wabunge kutoka Ujerumani. Kutoka kushoto ni Balozi Dora Msechu, Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika,Bibi Zainab Angovi, Afisa kutoka Idara ya Ulaya na Amerika na Bw. Grayson Ishengoma, Afisa kutoka Idara ya Ulaya na Amerika.

Mhe. Membe akifurahia Medali Maalum aliyokabidhiwa na Mhe. Willsch kama ishara ya kutambua ushirikiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Ujerumani.

Mhe. Membe akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe huo.No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.