Follow by Email

Wednesday, January 9, 2013

Waziri Membe apokea Nakala ya Hati za Utambulisho za Balozi Mteule wa Msumbiji nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe-Mb., akipokea Nakala ya Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Msumbiji hapa nchini Mhe.Vicente M. Veloso. Hafla hiyo ilifanyika Ofisini kwa Mhe. Waziri Membe leo. 

Mhe. Balozi Veloso aliye kushoto akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John M. Haule huku Mhe. Membe akishuhudia.

 Mhe. Membe akifafanua jambo kwa Mhe. Balozi Veloso wakati wa mazungumzo yao mara baada ya Balozi huyo kuwasilisha Nakala ya Hati zake za Utambulisho 

Mhe. Membe akimsikiliza Balozi Veloso huku Afisa kutoka Ubalozi wa Msumbiji hapa nchini, Bi. Helena Sitore akinukuu mazungumzo yao.


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.