Follow by Email

Thursday, January 17, 2013

TAARIFA KWA WATANZANIA WAISHIO MAENEO YA UWAKILISHI WA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI AFRIKA KUSINI

                                                                

TAARIFA KWA WATANZANIA WAISHIO KATIKA MAENEO YA UWAKILISHI WA UBALOZI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NCHINI AFRIKA KUSINI

Mhe. Radhia N.M. Msuya, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Afrika Kusini anawatangazia watanzania wote waishio katika maeneo ya uwakilishi wa Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Afrika Kusini yaani Afrika Kusini, Lesotho, Botswana na Namibia kuwa wanaombwa kujiandikisha kupitia anuani ya Ubalozi ifuatayo: administration@tanzania.org.za ili kurahisisha msaada wakati watanzania wanapopatwa na shida mbali mbali.

Sambamba na taarifa hii, Mheshimiwa Balozi anapenda kuzishukuru Jumuiya za watanzania waishio katika maeneo ya uwakilishi wake kwa ushirikiano wa dhati wanaoutoa kwa Ubalozi wao katika kutekeleza majukumu yake ya kila siku ya kuimarisha mashirikiano na nchi za uwakilishi huo.

Tunawashukuru na kuwatakia heri ya mwaka mpya, 2013!

Ahsanteni.

Imetolewa na,

Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Pretoria,
JAMHURI YA AFRIKA KUSINI

17 Januari, 2013


Unapojibu tafadhali taja:
TZPR/I.20/I 

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.