Follow by Email

Tuesday, January 15, 2013

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


220px-Coat of arms of Tanzania.svg f1f71


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Benin ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (UA), Mhe. Boni Yayi anatarajiwa kuwasili hapa nchini leo Jumanne tarehe 15 Januari, 2013 saa 2.00 usiku kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.

Mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Mhe. Yayi atapokelewa na Mwenyeji wake Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Akiwa nchini Mhe. Yayi anatarajiwa kufanya mazungumzo na mwenyeji wake Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Ikulu, Dar es Salaam tarehe 16 Januari, 2013 ambapo mbali na kuzungumzia masuala ya ushirikiano kuhusu nchi hizi mbili, viongozi hawa watazungumzia masuala muhimu kuhusu Bara la Afrika.

Mhe. Yayi alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika wakati wa Mkutano wa 18 wa Wakuu wa Nchi wa Umoja huo   uliofanyika Addis Ababa, Ethiopia mwezi Januari 2012 na atamaliza muda wake wa uenyekiti wakati wa Mkutano wa 20 wa Wakuu wa Nchi wa Umoja huo utakaofanyika Addis Ababa tarehe 27 na 28 Januari 2013.

Mhe. Yayi anatarajiwa kuondoka nchini tarehe 16 Januari 2013.
Imetolewa na:

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,

Dar es Salaam.

15 Januari, 2013.

  

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.