Follow by Email

Friday, January 11, 2013

Rais wa Madagascar awasili kuhudhuria mkutano wa SADC-TROIKA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), (kushoto) akisalimiana na Mhe. Andry Rajoelina, Rais wa Madagascar mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam tarehe 11 Januari, 2013. Mhe. Rais Rajoelina yupo nchini  kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano unaoendelea wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC-TROIKA).
Mhe. Rais Rajoelina akisalimiana na Viongozi mbalimbali mara baada ya kuwasili.
Mhe. Rais Rajoelina akiwa amefuatana na Mhe. Membe mara baada ya kupokelewa.
Mhe. Rais Rajoelina akipita katikati ya Gwaride  lililoandaliwa kwa heshima yake huku akisindikizwa na Mhe. Membe
Mhe. Rais Rajoelina akiwa na Mhe. Membe wakifurahia burudani ya ngoma za utamaduni zilizokuwepo Uwanjani hapo mara baada ya kuwasili.


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.