Follow by Email

Monday, January 21, 2013

Rais Kikwete ziarani Ufaransa; aambatana pia na Waziri Membe


Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akikagua gwaride lililoandaliwa rasmi kwa heshima yake na Rais Francois Hollande wa Ufaransa, mapema leo mjini Ufaransa.  Mhe. Rais Kikwete yuko nchini Ufaransa kwa ajili ya ziara ya kiserikali ya siku tano. 

Mhe Rais Kikwete akilakiwa na mwenyeji wake Mhe. Rais Francois Hollande wa Ufaransa katika Ikulu ya nchi hiyo maarufu kama Champs L'Elyesee mapema leo jijini Paris. 

Rais Kikwete (wa tatu kushoto) pamoja na ujumbe wake kutoka Tanzania, wakiwa katika mazungumzo rasmi na mwenyeji wake Rais Francois Hollande wa Ufaransa na ujumbe wake.  Mazungumzo hayo yalifanyika mapema leo katika Ikulu ya champs L'Elysee jijini Paris.  Mwingine katika picha ni Mhe. Waziri Bernard K. Membe (Mb) (wa pili kushoto), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.    

Rais Francois Hollande wa Ufaransa akimsindikiza Rais Kikwete wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mara baada ya kumaliza mazungumzo yao mapema leo katika Ikulu ya nchi hiyo. 

Rais Kikwete na mwenyeji wake Rais Francois Hollande wa Ufaransa wakiongea na waandishi wa habari mara baada ya mazungumzo yao.  (PICHA NA IKULU)


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.