Follow by Email

Friday, January 25, 2013

Mhe. Waziri Membe afanya mazungumzo na Katibu Mtendaji wa SADC


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, (kushoto) Mhe. Bernard K. Membe (Mb) akibadilishana mawazo na Katibu Mtendaji (kulia) wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) walipokutana nchini Ethiopia katika mkutano wa AU.

Mhe. Membe anasisitiza jambo wakati alipokuwa anafanya mazungumzo na Katibu Mtendaji wa SADC, anayefuata baada ya Mhe. Waziri ni Mhe. Joram Biswaro, Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia na Balozi Vincent Kibwana, Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Mhe. Waziri Bernard Membe (kulia) akisikiliza jambo kutoka kwa Mhe. Joram Biswaro, Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia nje ya ukumbi wa mkutano mjini Addis Ababa. mwingine katika picha ni mmoja wa ujumbe wa Tanzania katika mkutano wa AU.No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.