Follow by Email

Thursday, January 10, 2013

Marais wa SADC-TROIKA wawasili nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) (kushoto) akisalimiana na Mhe. Armando Emillio Guebuza, Rais wa Msumbiji mara baada ya Rais huyo kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo. Mhe. Guebuza ni miongoni mwa Marais wanaohudhuria Mkutano Maalum wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC-TROIKA) unaofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 10 Januari, 2013.

Mhe. Guebuza (kushoto) akifuatana na Waziri Membe mara baada ya kuwasili

Mhe. Rais Guebuza wakati alipokuwa akiteremka kwenye ndege mara baada ya kuwasili nchini.


Mhe. Rais Guebuza akiangalia ngoma za utamaduni (hazipo pichani) zilizokuwa zikitoa burudani kiwanjani hapo mara baada ya kuwasili.

Moja ya kikundi cha utamaduni kilichokuwa kikitoa burudani kwa Mhe. Rais Guebuza alipowasili nchini.


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.