Follow by Email

Saturday, December 8, 2012

Wakuu wa Nchi za SADC washiriki hafal ya chakula cha jioni

kwa
Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwakaribisha Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) kwenye Hafla ya Chakula cha Jioni aliyoiandaa kwa heshima yao iliyofanyika katika Hoteli ya Serena Jijiji Dar es Salaam tarehe 7 Desemba, 2012. Wakuu hao wa nchi wapo nchini kuhudhuria mkutano wa SADC utakaojadili masuala mbalimbali ya kikanda.
Wakuu wa Nchi za SADC wakiwa na mwenyeji wao Mhe. Rais Kikwete wakati wa Hafla ya Chakula cha Jioni.
Wakuu wa Nchi za SADC wakiwa katika ukumbi wa Serena walipofika kwa ajili ya hafla ya chakula cha jioni jana. Kutoka kushoto ni Mhe. Jacob Zuma, Rais wa Afrika Kusini, Mhe. Joseph Kabila, Rais wa DRC, Mhe. Armando Guebuza, Rais wa Msumbiji na Mhe. Hifikepunye Pohamba, Rais wa Namibia.

Maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakiwa Hotelini hapo kutekeleza majukumu ya kiitifaki ya kuhudumia wajumbe wa mkutano.


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.