Follow by Email

Saturday, December 8, 2012

Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC waanza

Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Dkt. Tomaz Augusto Salomao akiwakaribisha wajumbe (hawapo pichani) kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya hiyo uliofanyika kwenye Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam tarehe 8 Desemba, 2012.

Rais wa Msumbiji na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Mhe. Armando Guebuza akifungua rasmi Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya hiyo uliofanyika katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam tarehe 8 Desemba, 2012. Wengine katika picha ni Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete (wa pili kutoka kushoto), Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Yoweri Museveni (kulia), Rais wa Uganda na Mwenyekiti wa Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu (ICGLR) na Dkt. Salomao (kushoto), Katibu Mtendaji wa SADC.

Baadhi ya Wajumbe kwenye mkutano wa SADC wakisiliza hotuba ya ufunguzi wa mkutano huo kutoka kwa Mhe. Rais Guebuza (hayupo pichani).

Mhe. Yoweri Museve (Kulia), Rais wa Uganda na Mwenyekiti wa Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu  (ICGLR) akihutubia mkutano wa Wakuu wa Nchi wa SADC. Wengine katika picha wanaosikiliza ni Mhe. Rais Kikwete (wa pili kutoka kushoto), Mhe. Rais Guebuza (wa pili kutoka kulia) na Dkt. Salamao (kushoto).


Rais Guebuza (kushoto) ambaye ni Mwenyekiti wa SADC akiteta jambo na Mhe. Rais  Museveni (kulia) ambaye pia ni Mwenyekiti wa ICGLR wakati wa mkutano wa SADC.

Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) (wa pili kushoto), Waziri  wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akiwa na wajumbe wengine wakati wa mkutano wa SADC.

Mhe. Rais Kikwete (kushoto) akishauriana jambo na Mhe. Bernard K. Membe (Mb) (katikati), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa pamoja na Mhe. Shamsi Vuai Nahodha, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa mara baada ya ufunguzi rasmi wa  mkutano wa SADC.

Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya mkutano huo kufunguliwa rasmi katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam tarehe 8 Desemba, 2012.


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.