Follow by Email

Monday, December 17, 2012

Mhe. Mahadhi akabidhi Kibali cha Uwakilishi

Mhe. Mahadhi Juma Maalim (Mb), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akisalimiana na Bibi Rima Yassine Khalaf, Mwakilishi wa Heshima wa Serikali ya Senegal nchini Tanzania walipokutana ofisini kwa Naibu Waziri leo.

Mhe. Naibu Waziri akimkabidhi Kibali Bibi Khalaf ili aweze kutekeleza majukumu yake ya Uwakilishi wa Heshima wa Serikali ya Senegal nchini Tanzania.

Mhe. Naibu Waziri na Bibi Khalaf wakiwa katika mazungumzo mara baada ya zoezi la makabidhiano ya Kibali kukamilika

Mazungumzo yakiendelea huku Bibi Mercy Kitonga wa kwanza kushoto na Bw. Selestine Kakele wa kwanza kulia wote ni Maafisa wa Mambo ya Nje wakisikiliza kwa makini.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.