Follow by Email

Thursday, November 1, 2012

Naibu Waziri atembelea Ubalozi wa Tanzania nchini India

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Mahadhi Juma Maalim (Mb.), akisaini Kitabu cha Wageni  alipotembelea Ubalozi wa Tanzania nchini India. Anayeshuhudia pembeni ni Mhe. John Kijazi, Balozi wa Tanzania nchini humo. Mhe. Maalim yupo nchini India kuhudhuria Mkutano wa Mawaziri wa Nchi zinazopakana na Bahari ya Hindi (Indian Ocean Rim).

Mhe. Maalim akimsikiliza Balozi Kijazi wakati akimkaribisha  kuzungumza na Watumishi wa Ubalozini. Wengine katika picha ni baadhi ya Watumishi wa Ubalozi huo.

Mhe. Maalim (mwenye tai ya bluu) akiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Balozi Kijazi  (kulia kwake) na Watumishi wa Ubalozi wa Tanzania uliopo New Delhi nchini India mara baada ya kuwatembelea na kuzungumza nao.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.