Follow by Email

Saturday, November 3, 2012

Naibu Waziri ashiriki Mkutano wa IOR na kukutana na baadhi ya Mawaziri kwa mazungumzo

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Mahadhi Juma Maalim (kushoto) akiwa katika mazungumzo na Mhe. Pierrot Jocelyn Rajaonarivelo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Madagascar. Mhe. Maalim na Mhe. Rajaonarivelo wapo nchini India kuhudhuria Mkutano wa Mawaziri kutoka Nchi Zinazopakana na Bahari ya Hindi (Indian Ocean Rim-IOR)

Mhe. Maalim akisalimiana na Mhe. Abu-Bakr Al-Qirbi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Yemen wakati wa Mkutano wa Mawaziri kutoka Nchi Zinazopakana na Bahari ya Hindi unaoendelea nchini India

Mhe. Maalim akipata picha ya kumbukumbu  na Mhe. Jean-Paul Adam, Waziri wa Mambo ya Nje wa Shelisheli mara baada ya kumaliza mazungumzo yao. Mawaziri hao wapo nchini India kuhudhuria Mkutano wa Nchi zinazopakana na Bahari ya Hindi.

Mhe. Maalim (katikati) katika picha ya pamoja na  Mhe. Jean-Paul Adam (wa pili kutoka kushoto), Waziri wa Mambo ya  Nje wa Shelisheli na Mhe John Kijazi (wa pili kutoka kulia), Balozi wa Tanzania nchini India  na wajumbe wengine wanaoshiriki Mkutano wa Mawaziri wa Nchi zinazopakana na Bahari ya Hindi.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.