Follow by Email

Friday, November 23, 2012

Mkurugenzi wa Idara ya Asia azungumza na Makamu wa Rais wa Kampuni ya Sumitomo ya Japan

Balozi Mbelwa Kairuki (kulia), Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akimkaribisha Wizarani Bw. Hitokazu Okado, Makamu wa Rais wa  Kampuni ya Sumitomo ya Japan alipofika kwa mazungumzo kuhusu masuala mbalimbali ya uwekezaji.
Balozi Mbelwa akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo yake na Bw. Okado.
Bw. Okado akimuelezea Balozi Kairuki shughuli mbalimbali zinazofanywa na Kampuni ya Sumitomo.
Balozi Kairuki (wa tatu kutoka kulia) akimsikiliza Bw.Okado  (wa pili kutoka kushoto) wakati wa mazungumzo yao. Wengine katika picha ni Bw. Tetsujiro Tani ( kushoto) Mkurugenzi Msaidizi wa Kampuni  ya Sumitomo, Bi. Redemptor Tibaigana (Kulia), Afisa kutoka Idara ya Asia na Australasia, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Bw. Hasnein GulamHussein, Mkurugenzi wa Kampuni ya Sumitomo hapa nchini.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.