Follow by Email

Friday, November 23, 2012

Mkurugenzi wa Asia akutana na Mwakilishi wa Kampuni ya NEC Afrika kutoka Japan

Balozi Mbelwa Kairuki (kulia), Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akimkaribisha Wizarani Bw. Koji Nakamura, Mkurugenzi wa Kampuni ya NEC Afrika ya Japan inayojishughulisha na masuala ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano. Bw. Nakamura alifika Wizarani kwa lengo la kuitambulisha teknolojia mpya  inayotumiwa na Kampuni yake ikiwa ni jitihada za kuimarisha sekta ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano hapa nchini.

Balozi Kairuki akiwa katika mazungumzo na Bw. Nakamura kuhusu masuala ya Teknolojia hapa nchini.

Balozi Kairuki akimsikiliza Bw. Nakamura alipokuwa akimuelezea masuala mbalimbali kuhusu teknolojia hiyo.

Bw. Nakamura akimuonyesha Balozi Kairuki moja ya teknolojia wanayoitumia katika masuala mbalimbali ya mawasiliano.

Bw. Ryoji Metsuoka (kushoto), mmoja wa Wataalam aliyefuatana na Bw. Nakamura (katikati) akifafanua jambo kwa Balozi Kairuki kuhusu Teknolojia hiyo ya kisasa ya mawasiliano. 

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.