Follow by Email

Wednesday, November 14, 2012

Katibu Mkuu akutana na Mjumbe Maalum kutoka Argentina

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John M. Haule, akipokea Ujumbe Maalum kutoka Serikali ya Argentina kwa niaba ya Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kutoka kwa Balozi Bibiana Jones. Balozi Jones ni Mkurugenzi wa Idara ya Afrika anayeshughulikia nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Argentina.

Bw. Haule akizungumza na Balozi Jones mara baada ya kupokea Ujumbe Maalum.

Balozi Jones akifafanua jambo kwa Bw. Haule wakati wa mazungumzo yao.

Katibu Mkuu, Bw. Haule akiendelea na mazungumzo na Balozi Jones kuhusu ushirikiano baina ya Tanzania na Argentina. Mwingine katika picha ni Balozi Dora Msechu, Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Katibu Mkuu akimsikiliza Balozi Jones wakati wa mazungumzo yao huku Balozi Msechu na Bi. Upendo Mwasha, Afisa katika Idara ya Ulaya na Amerika wakishuhudia.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.