Follow by Email

Saturday, October 13, 2012

Mhe. Rais Kikwete apokea Hati za Utambulisho za Balozi wa Cuba hapa nchini

Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete (kushoto), Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Mhe. Jorge Luis Lopez Tormo, Balozi mpya wa Jamhuri ya Cuba hapa nchini.Hafla hiyo ilifanyika Ikulu, Dar es Salaam jana.

Mhe. Rais Kikwete akimtambulisha Mhe. Mahadhi Juma Maalim (kushoto wanaosalimiana), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa Mhe. Balozi Tormo. Anayeshuhudia pembeni mwa  Mhe. Naibu Waziri ni Bibi Grace Shangali, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Mhe. Rais Kikwete akizungumza na Mhe. Balozi Tormo mara baada ya kupokea Hati za Utambulisho za Balozi huyo. Pembeni mwa Balozi ni Mke wake Bibi Maria Griselda Herviz.

Mhe. Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Balozi Tormo na mkewe Bibi Herviz mara baada ya kupokea hati za utambulisho za Balozi huyo.

Mhe. Balozi Tormo akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili Ikulu.

Mhe. Balozi Tormo akisikiliza Wimbo wa Taifa lake uliokuwa ukipigwa na Bendi ya Polisi (haipo pichani) kwa heshima yake mara baada ya kuwasili Ikulu kwa ajili ya kuwasilisha Hati za Utambulisho kwa Mhe. Rais. Wengine katika picha ni Bw. Shaaban Gurumo (kulia kwa Balozi), Mnikulu na Bw. Japhet Mwaisupule (kushoto kwa Balozi), Kaimu Mkuu wa Itifaki.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.