Follow by Email

Wednesday, September 5, 2012

MKUTANO WA WARATIBU NA WATAALAM WA NCHI ZA MAZIWA MAKUU (ICGLR)‏


Balozi James Mugume, Mratibu wa Kitaifa kutoka Uganda ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mkutano wa Waratibu wa Kitaifa na Wataalam kutoka Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu akifungua mkutano huo leo tarehe 5 Septmba, 2012 uliofanyika katika Hoteli ya Speke Resort iliyopo eneo la Munyonyo pembezoni mwa Jiji la Kampala, Uganda. Mkutano huo utafuatiwa na Mkutano wa Mawaziri tarehe 6 Septemba, 2012 na baadaye Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali utakaofanyika Kampala, Uganda tarehe 7 na 8 Septemba, 2012.


Prof. Ntumba Luaba, Katibu Mtendaji wa Sekretarieti ya Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu akihutubia mkutano wa Waratibu wa Kitaifa na Wataalam kutoka nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu uliofanyika leo katika Hoteli ya Speke Resort, Munyonyo.


Bw. Samwel Shelukindo, Mjumbe kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Tanzania akisikiliza kwa makini hotuba iliyokuwa inatolewa na Katibu Mtendaji wa Sekretarieti ya Maziwa Makuu (hayupo pichani) wakati wa Mkutano wa Waratibu wa Kitaifa na Wataalam kutoka nchi za Maziwa Makuu uliofanyika jijini Kampala, Uganda.


Baadhi ya Wajumbe kutoka Tanzania wakinukuu taarifa muhimu wakati wa Mkutano wa Waratibu wa Kitaifa na Wataalam kutoka nchi za Maziwa Makuu unaondelea jijini Kampala, Uganda.


Picha ya pamoja ya Waratibu wa Kitaifa na Wataalam kutoka nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu waliohudhuria mkutano wao.
Picha zote na Rosemary Malale


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.