Follow by Email

Thursday, September 6, 2012

MKUTANO WA KAMATI YA MAWAZIRI WA MAZIWA MAKUU WAFANYIKA, KAMPALAMhe. Okello Oryem, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mawaziri wa Mambo ya Nje na wa Ulinzi wa Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu (RIMC) akifungua mkutano wa Mawaziri hao uliofanyika mjini Kampala, Uganda leo. Kushoto kwa Mhe. Oryem ni Prof. Ntumba Luaba, Katibu Mtendaji wa Sekretarieti ya Maziwa Makuu na kulia kwa Mhe. Oryem ni Makamu Mwenyekiti.


 Kiongozi wa Ujumbe wa Tanzania kwenye mkutano wa Kamati ya Mawaziri wa Mambo ya Nje na Ulinzi wa Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu, Mhe. Shamsi Vuai Nahodha, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (kushoto) akiwa  na Mhe. Balozi Rajab Gamaha, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakati wa mkutano wa kamati hiyo uliofanyika mjini Kampala, Uganda leo.

Baadhi ya wajumbe kutoka Tanzania wakiwa katika mkutano wa Kamati ya Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu uliofanyika leo mjini Kampala, Uganda. Kutoka kulia ni Mhe. Ladislaus Komba, Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Balozi Naimi Aziz, Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikaino wa Kikanda, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Bw. Samwel Shelukindo, Afisa Mwandamizi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.Picha zote na Rosemary Malale


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.