Follow by Email

Wednesday, August 8, 2012

Rais Kikwete arejea nchini kutoka UgandaMhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete amerejea nchini jioni hii mara baada ya kuhudhuria Mkutano Maalum wa Wakuu wa Nchi za Maziwa Makuu uliofanyika kuanzia tarehe 7 hadi 8 Agosti, 2012 mjini Kampala, Uganda.  Agenda kuu ya Mkutano huo ilikuwa ni kutafuta njia ya amani ya kusuluhisha mgogoro unaondelea Mashariki ya nchi ya Kongo DRC.  Rais Kikwete alipokelewa na Mhe. Bernard K. Membe (MB) (kulia), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Dkt. Didas Masaburi, Meya wa jiji la Dar es Salaam kwenye Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere. Aidha, Mkutano huo ulihudhuriwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Shamsi Vuai Nahodha (MB)(Picha na Freddy Maro) 

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.