Follow by Email

Friday, August 31, 2012

ANGOLA WAFANYA UCHAGUZI MKUU LEO


Mhe. Bernard K. Membe (MB), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa nchini Tanzania, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC, akiongea na wadau wakati zoezi la upigaji kura likiendelea jijini Luanda, nchini Angola.


Mhe. Waziri Membe akitembelea moja ya vituo vya kupigia kura nchini Angola.ANGOLA WAFANYA UCHAGUZI MKUU LEO

Wananchi wa Angola leo wanafanya uchaguzi Mkuu wa pili tangu kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe.  Uchaguzi Mkuu huo wa Wabunge na Rais unahusisha vyama vya siasa.  Vyama vikubwa vya siasa ni chama tawala MPLA na chama kuku cha upinzani UNITA.

Tanzania inaangoza timu ya waangalizi wa uchaguzi wa SADC chini ya uenyekiti wa Mhe Bernard K. Membe, Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC, Timu ya SADC inahusisha waangalizi 110 wa Uchaguzi kutoka nchi za SADC wakiweko 13 kutoka Tanzania.

Hadi sasa zoezi la upigaji kura limefanyika kwa amani na utulivu na watu wengi wamejitokeza kupiga kura katika jiji la Luanda na viunga vyake.

Zoezi la upigaji kura bado linaendelea.


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.