Follow by Email

Tuesday, July 24, 2012

WAZIRI MEMBE ATOA MKONO WA POLE


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dk.Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimatifa, Mhe. Benard K. Membe (MB).  Waziri Membe alifika Ikulu Mjini Zanzibar
jana, kwa madhumuni ya kutoa mkono wa pole kwa Rais kutokana na Ajali ya
Meli ya Mv Skagit ya Kampuni ya Seagul, na kusababisha wananchi kupoteza
Roho zao.  [Picha na Ramadhan Othman,Ikulu Zanzibar.]


 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,
Dk.Ali Mohamed Shein, akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimatifa, Mhe. Benard K. Membe (Mb), baada ya Waziri Membe kufika
Ikulu Mjini Zanzibar jana.  Waziri Membe alimtembelea Mhe. Rais Shein kwa madhumuni ya kutoa mkono wa pole kutokana na Ajali ya Meli ya Mv Skagit ya Kampuni ya Seagul.  [Picha na Ramadhan Othman,Ikulu Zanzibar.]Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd akiwa katika mazungumzo na Mhe. Waziri Bernard K. Membe (MB), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.  Mhe. Membe alikuwa Mjini Zanzibar kumpa salamu za pole Balozi Idd kutokana na ajali ya Meli ya MV Skagit iliyotokea wiki iliyopita.  [Picha na Ramadhan Othman,Ikulu Zanzibar.]

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.