Follow by Email

Wednesday, July 18, 2012

Uteuzi wa Dkt. Wilbald Lorri kuwa Msaidizi wa Rais, Masuala ya Lishe

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS


Telephone: 255-22-2114512, 2116898
              press@ikulu.go.tz             

Fax: 255-22-2113425


PRESIDENT’S OFFICE,
      THE STATE HOUSE,
              P.O. BOX 9120,  
DAR ES SALAAM.
Tanzania.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Dkt. Wilbald Lorri kuwa Msaidizi wa Rais, Masuala ya Lishe (Nutrition).
Taarifa iliyotolewa leo, Jumatano, Julai 18, 2012 na Ofisi ya Katibu Kiongozi (KMK), Balozi Ombeni Sefue, kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, inasema kuwa uteuzi huo wa Dkt. Lorri ulianza tokea Juni Mosi, 2012.
Kabla ya uteuzi wake, Dkt. Lorri ambaye ana shahada ya uzamivu (PhD) katika Sayansi ya Lishe alikuwa mtaalam wa lishe katika Mradi wa Feed the Future unaoendeshwa nchini na Shirika la Maendeleo la Marekani  - USAID.
Aidha, kati ya mwaka 1994 na 2003, Dkt Lorri alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Lishe Tanzania – (Tanzania Food and Nutrition Centre).

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
18 Julai, 2012

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.