Follow by Email

Monday, July 9, 2012

Rais Kikwete akabidhi Tuzo ya Heshima ya Juu ya Burundi

Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo amemkabidhi Mama Maria Nyerere Tuzo ya Juu ya Heshima ya Taifa la Burundi aliyotunukiwa Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.  Tuzo hiyo ilitunukiwa wakati wa maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru wa Burundi yaliyofanyika mjini Bujumbura wiki iliyopita.   Mwalimu Nyerere alitunukiwa tuzo hiyo kwa mchango wake wakati wa harakati kupigania uhuru wa Burundi ambapo alikuwa mshauri wa karibu wa Waziri Mkuu wa Kwanza wa nchi hiyo ya Prince Louis Rwagasore.   (Picha na Freddy Maro)


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.