Follow by Email

Tuesday, July 10, 2012

Mhe. Dkt. Asha-Rose Migiro arejea nchini


Baadhi ya Mabalozi, Wahadhiri na Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam pamoja na wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakiwa wamejipanga kumpokea Dr. Asha Rose Migiro.


Mhe. Dkt. Asha-Rose Migiro aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akiteremka katika gari lililofika kumpokea mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam jana akitokea New York, Marekani baada ya kumaliza muda wake wa kazi katika Umoja huo.


Mhe. Dkt. Migiro akisalimiana na baadhi ya Wakururugenzi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa walipofika kumpokea uwanjani hapo jana.Mhe. Dkt. Migiro akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani)  mara baada ya kuwasili nchini. Kulia kwake ni Mhe. Membe na kushoto ni Dkt. Alberic Kacou, Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa hapa nchini.

Dr. Asha Rose Migiro (katikati) akiteta jambo Waziri Membe sambamba na Viongozi mbalimbali wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini wakiongozwa na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dr. Alberi Kacou (kushoto) waliofika kumlaki katika Uwanja wa Ndege wa Mwl. J.K Nyerere.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.