Follow by Email

Tuesday, July 3, 2012

Maonesho Sabasaba

Maonesho ya 36 ya Biashara ya Kimataifa, yatafanguliwa leo rasmi saa nane mchana na Mhe. Balozi Seif Ali Idd, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwenye ukumbi wa Rashid Mfaume Kawawa katika Uwanja wa Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Aidha, Mhe. Balozi Idd anatarajiwa kutembelea mabanda mbalimbali wakati wa ufunguzi huo, wakati wageni waalikwa wanatakiwa kuanza kuwasili ukumbini saa saba mchana.
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa , ikishirikiana na Taasisi zake tatu, ambazo ni Taasisi ya Chuo cha Diplomasia cha Kurasini (CFR), Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC) na Mpango wa Kujitathmini Kiutawala Bora (APRM) zinashiriki  kwa mara nyingine katika maonesho hayo ya Biashara ya Kimataifa.   
Wizara itakuwa katika jengo la Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma.
Maonesho hayo yameanza rasmi  tarehe 28 Juni na yatamalizika tarehe 08 Julai 2012.  Wote mnakaribishwa.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.